Pages

Saturday, 4 April 2015

MECHI ZOTE ZA LEO ZITASIMAMA DAKIKA MOJA KUOMBOLEZA KUFUATIA AJALI ALIYOSABABISHA VIFO VYA MASHABIKI WA SIMBA UKAWA

Kufuatia vifo vya mashabiki wa Simba ,mechi zote za ligi wikiendi hii zitatanguliwa na dakika moja ya maombokezo.Mungu awarehemu.Mashabiki wa Simba Ukawa ambao wamefariki dunia katika ajali mbaya ya gari iliyotkea jana jioni nje kidogo ya mji wa Morogoro.
HILI NDILO GARI LILILOPATA AJALI JANA NA KUSABABISHA VIFO VYA MASHABIKI WA SIMBA 
Mashabiki wanne wa Simba Ukawa wamefariki dunia na watu wengine wawili walioelezwa kuwa ni abiria pia wamepoteza maisha.
Taarifa kutoka katika eneo la ajali zimeeleza mashabiki hao walikuwa njiani kwenda mjini Shinyanga kuishangilia Simba inayopambana na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kambarage.
Imeelezwa gari hilo aina ya Toyota Coaster limeacha njia ghafla na kuingia porini kabla ya kuanguka.
Baadhi ya majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro na wanapata matibabu huku mmoja wao akiwa taabani.
TFF imepokea kwa masikitiko taarifa za ajali iliyowakuta mashabiki wa Simba waliokuwa safarini jana.na kutoa pole kwa wafiwa wote.
Hata hivyo Rais wa TFF Jamal Malinzi ameagiza basi la TFF liende Morogoro lisaidie shughuli ya kusafirisha majeruhi na marehemu kupaleka Dar es salaam.

JUMA WALEO BLOG INATOA POLE KWA NDUGU JAMAA NA MASHABIKI WA SIMBA NA WAPENDA MICHEZO WOTE WALIOGUSWA NA VIFO HIVYO MUNGU AWAJAALIE MAJERUHI WAPONE HARAKA

Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates