Kocha wa Klabu ya Bundesliga ya Germany Borussia Dortmund, Jurgen Klopp, ametangaza kuachana na Klabu hiyo inayosuasua Msimu huu.
Kocha huyo ambae Mkataba wake ulikuwa unamalizika 2018 amesema ataondoka Klabuni hapo mwishoni mwa Msimu.
Klopp, mwenye Miaka 48, alijiunga na Dortmund Mwaka 2008 na kuiwezesha kutwaa Ubingwa wa Bundesliga Mwaka 2011 na 2012 ikiwa na pamoja na kutwaa Dabo akiweka rekodi ya kuwa Meneja wa kwanza wa Dortmund kufanya hivyo.
Pia Klopp aliiwezesha kufika Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo walifungwa 2-1 na Bayern Munich.
Pia Klopp aliiwezesha kufika Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo walifungwa 2-1 na Bayern Munich.
Hivi sasa Dortmund wako Nafasi ya 10 kwenye Bundesliga wakiwa Pointo 37 nyuma ya Mabingwa na Vinara wa Ligi hii ya Germany, Bayern Munich.
0 comments:
Post a Comment