Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, Azam FC, Leo wako huko Tanga kucheza na Mgambo JKT Uwanjani Mkwakwani wakiwania ushindi na kupunguza pengo la Pointi 8 kati yao na Vinara Yanga.
Yanga wanaongoza Ligi wakiwa na Pointi 46 wakifuatiwa na Azam FC, waliocheza Mechi 1 pungufu, wakiwa na Pointi 38.
Wikiendi iliyopita, Azam FC walipata pigo la kutetea Ubingwa wao baada ya kutoka Sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar huko Manungu, Morogoro na sasa inabidi washinde Mechi zao zote zilizobaki, ambazo ni pamoja na dhidi ya Yanga na Simba, ikiwa watataka kutwaa tena Ubingwa waliotwaa kwa mara ya kwanza Msimu uliopita..
Hata hivyo, Mgambo JKT ni Timu ngumu kwa Vigogo hasa wakicheza kwao Mkwakwani na Leo Azam FC wanatinga Mechi hii wakiwa na hatari ya kuwakosa Nyota wao kadhaa wenye maumivu ambao ni pamoja na John Bocco, Abdallah Heri, Kipre Tchetche, Aggrey Morris na David Mwantika ambae ana matatizo ya Kifamilia.
Mechi nyingine hii Leo iko huko Manungu, Morogoro wakati Mtibwa Sugar wataikaribisha Tanzania Prisons.
0 comments:
Post a Comment