Khamis Mcha Khamis ‘Viali’ ambaye ni mchezaji wa Azam FC, timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ na ile ya Muungano ‘Taifa Stars’, amefiwa na baba yake mzazi hapo jana. Mzee Mcha Khamis amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu akisumbuliwa na matatizo ya njia ya mkojo, taratibu za mazishi zinafanywa. Klabu inampa pole Viali na familia yake na kuwataka wawe na subra katika kipindi hiki kigumu.
Msiba huo umetokea siku chache baada ya kiungo wa Simba SC Jonas Mkude kufiwa na baba yake mzazi mzee Gerrard Mkude.
0 comments:
Post a Comment