Jana wakiwa nyumbani Signal Iduna Park, Borrusia Dortimund waliachwa mdomo wazi baada ya kuchapwa Bao 1-0 na Bayern Munich kwenye Mechi ya Bundesliga ambayo ina Jina la Ubatizo 'DER KLASSIKER' na kipigo hiki kikidhihirisha Msimu mbovu wa Borussia Dortmund wakibaki katikati ya Msimamo wa Ligi na Bayern kuelekea kutetea Taji lao.
Bao la ushindi la Bayern lilifungwa na Mchezaji wa zamani wa Dortmund Robert Lewandowski katika Dakika ya 36.
Ushindi huu umewapa Bayern uongozi wa Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Wolfsburg na Dortmund kubaki Nafasi ya 10.
0 comments:
Post a Comment