Ligi Kuu Vodacom ilieendelea jana kwa Mechi 3 huku Mechi moja Ambayo ilikuwa ichezwe Uwanja wa Kambarage huko Shinyanga kati ya Kagera Sugar na Simba kulazimika kuahirishwa kutokana na Mvua kubwa kufanya Uwanja ujae Maji.
KIKOSI CHA TIMU YA POLISI MOROGORO |
Mechi hii sasa imepangwa kuchezwa Jumatatu kwa vile Jumapili ipo Mechi nyingine ya Ligi Uwanjani hapo kati ya Stand United na Mtibwa Sugar.
huko Mkwakwani, Tanga, wenyeji Coastal Union walichapwa 1-0 na Tanzania Prisons.
Huko Mabatini, Mlandizi, Ruvu Shooting iliifunga Ruvu JKT 1-0 na huko Nangwanda, Mtwara, Ndanda FC na Mbeya City zilitoka 1-1.
Vinara wa Ligi hii, Yanga, na Timu inayowafuata, Azam FC, zote hazina Mechi Wikiendi hii baada ya Mechi kati yao kuahirishwa kwa vile Yanga walikuwa Nchini Zimbabwe kucheza Mechi ya Marudiano ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho ambapo timu ya yanga ilifungwa goli 1-0 na playinum fc na kusonga mbele kwa jumla ya magoli 5-2.
0 comments:
Post a Comment