Jose Mourinho, Meneja wa Mabingwa wapya wa England Chelsea, amesema kuutwaa Ubingwa huo hapo Jana ni zawadi yake kwa kuikabili hatari ya kurudi tena kuiongoza Chelsea kwa mara ya pili.
Mourinho alitwaa Ubingwa mara mbili katika Misimu ya 2004/5 na 2005/6 alipokuwa Meneja wa Chelsea kwa mara ya kwanza kati ya 2004 na 2007 na sasa kurudi tena 2013 na kuiwezesha Chelsea kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu England kwa mara ya 4 na mara ya kwanza tangu 2010.
Akiongea Jana baada ya Chelsea kuifunga Crystal Palace Bao 1-0 Uwanjani Stamford Bridge kwa Bao la Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA, Eden Hazard, na kutwaa Ubingwa huku wakiwa na Mechi 3 mkononi, Mourinho alisema: "Ukirudi kule ulikopata mafanikio unahatarisha mafanikio na historia yako lakini mimi nimeikabili hatari hiyo na sasa naweza kusema nimeshinda!"
Aliongeza: "Ningeweza kwenda Nchi nyingine yenye Ligi laini lakini nliamua kurudi kwenye Ligi ngumu ambako kabla nlikuwa na furaha!"
Kuhusu kubaki kwake Chelsea, Mourinho alisema hilo ataamua Mmiliki wa Klabu Roman Abramovitch
0 comments:
Post a Comment