Wekundu wa msimbazi Simba imewachapa Mabingwa wa zamani Azam FC Bao 2-1 na kujiletea matumaini makubwa ya kufuzu Nafasi ya Pili na hivyo kucheza Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho Mwakani.
Simba wapo Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 1 tu nyuma ya Azam FC walio Nafasi ya Pili nyuma ya Yanga ambao tayari wameshatwaa Ubingwa.
Ikiwa Jumatano Yanga wataifunga Azam FC au kutoka Sare, Simba wanaweza kuipiku Azam FC katika Mechi za mwisho za Ligi zitakazochezwa Jumamosi Mei 9.
Katika Mechi hiyo Simba walinufaika kwa kucheza na Mtu 10 Azam FC baada Kiungo wao Abubakar Salum kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 38.
Simba walitangulia kufunga kwa Bao la Ibrahim Ajibu, Dakika ya 47, na Mudathir Yahya kuisawazishia Azam FC Dakika ya 57 lakini Ramadhan Singano akapiga Bao la Pili na la ushindi kwa Simba katika Dakika ya 74.
KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR |
Huko Tanga, Coastal Union imeitandika Stand United Bao 3-1 na huko Manungu, Morogoro, Mtibwa Sugar imeichapa Ruvu Shooting 2-0.
0 comments:
Post a Comment