Hiyo Jumanne, huko Juventus Stadium Mjini Turin Nchini Italy, Mabingwa wa Italy, Juventus, ambao Juzi walitetea Taji lao kwa mara ya 4 mfululizo, watawakaribisha Mabingwa mara 10 wa UIaya, Real Madrid, ambao pia ndio Mabingwa Watetezi.
Jumatano huko Nou Camp Mjini Barcelona Nchini Spain, Wenyeji Barcelona wanaoongoza La Liga, watawakaribisha Mabingwa wa Germany Bayern Munich ambayo sasa ipo chini ya Kocha Pep Guardiola ambae alijizolea sifa kubwa kwa kutwaa Mataji kibao akiwa na Barcelona kabla kung'atuka Miaka michache iliyopita.
Marudiano ya Nusu Fainali hizi za UCL yatafanyika Wiki ijayo Jumanne na Jumatano, Mei 12 na 13.
0 comments:
Post a Comment