Jumanne Usiku, Uwanja wa Juventus Arena Jijini Turin Nchini Italy, utakuwa ni dimba la Mechi ya Nusu Fainali ya kwanza ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, kati ya Juventus na Mabingwa Watetezi wa Mashindano haya, Real Madrid.
Nusu Fainali nyingine ya UCL ni Jumatano huko Nou Camp Mjini Barcelona Nchini Spain, ambapo Wenyeji Barcelona wanaoongoza La Liga, watawakaribisha Mabingwa wa Germany Bayern Munich ambayo sasa ipo chini ya Kocha Pep Guardiola ambae alijizolea sifa kubwa kwa kutwaa Mataji kibao akiwa na Barcelona kabla kung'atuka Miaka michache iliyopita.
Marudiano ya Nusu Fainali hizi za UCL yatafanyika Wiki ijayo Jumanne na Jumatano, Mei 12 na 13.
TATHMINI-Juventus v Real Madrid
Wenyeji Juventus wapo Nusu Fainali yao ya kwanza ya Mashindano haya tangu 2002/3 walipowatoa Real Madrid na kutinga Fainali waliyotoka Sare 0-0 na AC Milan Uwanjani Old Trafford na kubwagwa kwa Penati.
Real Madrid wao wanasaka kuwa Timu ya kwanza kuweza kutetea Taji lao la UCL tangu 1990 wakati AC Milan walipofanya hivyo kwenye Mashindano yaliyokuwa na mfumo tofauti na yaliyokuwa yakiitwa Kombe la Ulaya.
Juve na Real zipo miongoni mwa Timu 6 Bora katika Historia za UCL na Kombe la Ulaya.
Hali za WAchezaji
JUVENTUSMabingwa hawa wa Italy watawakosa Paul Pogba, Martin Caceres na Kwadwo Asamoah kutokana na Majeruhi.
Real Madrid
Real watawakosa Majeruhi Karim Benzema na Luka Modric na pia Sami Khedira ambae hakuwekwa Kikosini.
Dondoo Muhimu
Timu hizi zimekutana mara 16 kwenye Mashindano haya na Real kushinda mara 8, Juve 7 na Sare 1.CREDIT: SOKA IN TANZANIA

0 comments:
Post a Comment