Pages

Tuesday, 24 March 2015

KESHO MCHEZO MMOJA TU LIGI KUU TANZANIA BARA YANGA KUWAWINDA JKT RUVU TAIFA

LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ianatrajiwa kuendelea kesho (jumatano) kwa mchezo mmoja kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kwa wenyeji JKT Ruvu kuwakaribisha vinara wa ligi hiyo timu ya Yanga SC.

Yanga SC itahitaji ushindi katika mchezo huo, ili kuzidi kupiga kasi katika marathoni ya ubingwa wa Ligi Kuu.
A
Hadi sasa, ikiwa na pointi 37 baada ya kucheza mechi 18, Yanga SC ipo kileleni mwa Ligi Kuu, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi 36 za mechi 18 pia.
Share:

ANGALIA MSIMAMO WA LIGI KUU VODACOM


Share:

TIMU YA TAIFA YA MALAWI KUWASILI TANZANIA ALHAMISI HII

Msafara wa watu 25 wa timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) unatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam siku ya alhamis, kabla ya kuunganisha ndege siku ya ijumaa kuelekea jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Taifa Stars siku ya jumapili.
Katika msafara huo utakaokuwa na wachezaji 18 na viongozi 7, kocha mkuu wa The Flames Young Chimodzi amewajumuisha wachezaji nane (8) katika kikosi chake wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.
Wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini ni Limbikani Mzava (Celtic), Harry Nyirenda (Black Leopards), Esau Kanyenda (Polokwane City), na Atusaye Nyondo (University of Pretoria).
Wengine ni Nahodha Joseph Kamwendo (Tp Mazembe - Congo DR), Frank Banda (HBC Songo - Msumbuji), Chimango Kayira (Costal De Sol - Msumbuji) na Gerald Phiri (Caps United - Zimbambwe).

Share:

TAIFA STARS YAWASILI MWANZA TAYARI KUWAWINDA MALAWI JUMAPILI

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili salama leo asubuhi jijini Mwanza, tayari kwa maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa Kimataifa siku ya jumapili Machi 29, 2015 dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi (The Flames), mechi itakayochezwa kwenye dimba la Uwanja wa CCM Kirumba.
Kikosi cha Stars kimeondoka kikiwa na wachezaji 18 ambao wameripoti kambini jana, huku kiugo mshambuliaji Mwinyi Kazimoto anayecheza soka la kulipwa nchini Qatar akitarajiwa kuungana na wenzake leo mchana jijini Mwanza.
Wachezaji waliopo kambini jijini Mwanza ni, magolikipa Aishi Manula na Mwadini Ali (Azam FC), walinzi ni Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, Aggrey Morris (Azam FC) , Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Haji Mwinyi (KMKM), Hassan Isihaka na Abdi Banda (Simba SC)
Wengine ni Amri Kiemba, Frank Domayo, Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Haroun Chanongo (Stand United), John Bocco (Azam FC), Juma Luizio (Zesco United), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe).
Mchezaji Mcha Khamis wa Azam FC amjiondoa kikosini kutokana na kuwa majeruhi, huku wachezaji wa Young Africans wakitarajiwa kujiunga na kikosi hicho cha timu ya Taifa mara tu baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya JKT Ruvu siku ya jumatano.

Share:

Monday, 23 March 2015

JUMA NYOSSO KUMALIZA KIFUNGO CHA MECHI 8 KWENYE MECHI MBEYA CITY VS AZAM FC

Mlinzi wa kutumainiwa  wa City Juma Nyosso anatarajia kurejea  uwanjani kutumikia timu yake  kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Azam Fc uliopangwa kuchezwa Chamanzi Complex  mapema mwezi ujao.
Nyosso aliyekuwa akitumikia adhabu ya kufungiwa michezo 8 atakamilisha kifungo hicho jumamosi  ya tarehe 4.4 2015 wakati City itakapokuwa uwanjani kucheza na Ndanda Fc kwenye mchezo mwingine wa ligi hiyo utakaochezwa kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona  mkoni Mtwara.
JUMA NYOSSO WA PILI KUTOKA KUSHOTO
Akizungumza mapema leo Katibu Mkuu  City Emmanuel Kimbe amesema kurejea kundini kwa Nyosso kutaongeza nguvu kubwa kikosini hasa kwenye wakati huu ambao timu inafanya jitihada za dhati kupata matokeo ili kusaka nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.
“Kila mmoja hapa anayo kumbukumbu ya kazi nzuri aliyoifanya Nyosso kwenye mechi alizocheza kabla ya kupata adhabu, niseme wazi kuwa ni mchezaji muhimu ambaye uwepo wake unaongeza kitu, kila mmoja  anaweza kuitafsiri adhabu ile kwa namna yake, lakini uwanjani kuna mambo mengi, kuna wakati unaweza kufanya jambo usijue ulilifanya vipi, kizuri kwetu ni kuwa anamaliza adhabu hiyo na kurudi kuitumikia timu” alisema.
Wakati huo huo nyota wanaunda safu ya ushambuliaji  Paul Nonga, Mwegane Yeya na Themi Felix wamesema wako tayari kuwasha moto ndani ya uwanja wa Nangwanda sijaona kwa lengo moja tu la kuipatia   City ushindi kwenye mchezo dhidi ya ndanda fc.
Share:

YANGA YABAKIZA MECHI 8 MICHEZO SABA MFULULIZO WATACHEZA NYUMBANI

Baada ya juzi Jumamosi kufanikiwa kuifunga Mgambo JKT mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, sasa vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga, wamebakiza mchezo mmoja tu ambao ni sawa na dakika tisini, nje ya Jiji la Dar.


Yanga wamejikusanyia pointi 37 kwa kucheza michezo 18, wamebakiza michezo nane tu ili kuhitimisha ligi hiyo msimu huu ambayo inatarajiwa kufikia tamati Mei 9, mwaka huu.

Katika michezo hiyo nane, Yanga itacheza michezo saba mfululizo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar ambao wanautumia kwa michezo yao ya nyumbani huku ule wa mwisho wakilazimika kusafiri mpaka mkoani Mtwara kupambana na Ndanda FC kwenye Dimba la Nangwanda Sijaona.

Wakati Yanga ikiwa imebakiza mchezo mmoja ugenini, wapinzani wao wanaowafuatia kwa karibu, Azam nao pia wamebakiza mchezo mmoja dhidi ya Mtibwa Sugar huku Simba wao wakiwa wamebakiza michezo miwili ambapo watacheza dhidi ya Kagera na Mbeya City.

Yanga na Azam zina nafasi kubwa ya kulitwaa kombe hilo endapo tu zitatumia vizuri mechi hizo za nyumbani.
Share:

UMEISIKIA TAARIFA YA KIFO CHA MCHEZA MIELEKA ISOME HAPA

Mcheza mieleka maarufu wa Mexico Hijo del Perro Aguayo ambaye amepoteza maisha wakati alipodondoka jukwani akiwa katikati ya mchezo ikiwa ni saa chache baada ya kukimbizwa hospitali.
Mwanamieleka huyo alikuwa akipigana na mwezake Rey Mysterio katika pambano lililofanyika ijumaa usiku na mara baada ya kudondoka alikimbizwa hospitali lakini madaktari walithibitisha kuwa tayari amefariki.
Wakati akiwa amedondoka chini wenzake hawakujua kiasi gani ameumia na kuendelea na mchezo na baada ya dakika zipatazo mbili waligundua kuwa amezidiwa hivyo kumuwahisha hospitali.
Hapa kuna video ikionyesha wakati pambano hilo linafanyika hadi mwana mieleka huyo alipopoteza  fahamu akiwa ulingoni.
Share:

JOSE MOURIHNO "CHELSEA ILITAKIWA KUWA BINGWA MAPEMA KABISA"

Jose Mourinho anaamini Chelsea wapo njiani kutwaa Ubingwa baada ya Jana kupigana na kushinda 3-2 huko KC Stadium walipocheza na Hull City.
Ushindi huo, uliopatikana kwa Bao la 3 la Loic Remy baada ya Chelsea kuongoza 2-0 na Hull kurudisha na Gemu kuwa 2-2, umewafanya Chelsea wawe Pointi 6 mbele ya Man City huku wakiwa na Gemu 1 mkononi na sasa njia inazidi kufunguka kwao kutwaa Ubingwa wao wa kwanza tangu 2010.
Mourinho amesema: “Mbio za Ubingwa zilipaswa kuwa zimekwisha. Kwa hali ya kawaida, Chelsea walitakiwa wawe Pointi 8, 10, 12 au zaidi mbele. Lakini Soka haitabiriki na sasa tupo Pointi 6 mbele na ni nafasi safi kupita tulipokuwepo. Ninajiamini na naamini Wachezaji wangu!”
Share:

ALICHOKISEMA STEVEN GERRARD KUHUSU KADI NYEKUNDU ALIYOPEWA JANA

KEPTENI wa Liverpool Steven Gerrard ameomba radhi kwa kutandikwa Kadi Nyekundu Sekunde 38 tu baada ya kuingia Uwanjani kwenye Mechi iliyochezwa Anfield na Timu yake kutandikwa 2-1 na Manchester United hapo Jumapili.
Gerrard, mwenye Miaka 34 na ambae anahamia huko Marekani kuchezea LA Galaxy mwishoni mwa Msimu, alitolewa nje na Refa Martin Atkinson kwa kumkanyaga kusudi Ander Herrera wa Man United na sasa atakosa Mechi 3 za Liverpool.
Akiongea mara baada ya Mechi hiyo, Gerrard alisema: “Inabidi nikubali, uamuzi ulikuwa sahihi. Nimewaangusha Wachezaji wenzangu na Mashabiki. Nawajibika kwa yote. Hata sijui nini kilitokea labda kukumbwa na Herrera. Sisemi zaidi. Ila nimekuja hapa kuomba radhi.”
Wakati akipewa Kadi Nyekundu, Liverpool ilikuwa nyuma kwa Bao 1-0 na hii pengine ni Mechi yake ya mwisho dhidi ya Mahasimu Man United akiwa amevaa Jezi ya Liverpool Klabu ambayo alianza kuichezea tangu 1998 na kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2005 pamoja na Vikombe vingine 9.
Mechi ambazo atazikosa Gerrard akiwa kwenye Kifungo chake cha Mechi 3 ni ile ya huko Ewood Park dhidi ya Blackburn Rovers ya Marudiano ya Robo Fainali ya FA CUP, Mechi ya Ligi Kuu England huko Emirates na Arsenal na ile ya Anfield na Newcastle hizi zikiwa Mechi kati ya 8 walizobakisha za Ligi.
Share:

MALINZI AWAPONGEZA TWIGA STARS BAADA YA JANA KUIBOMOA SHEPOLOPOLO 4-2

 Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini –TFF Bw. Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia (The She-polopolo).
Katika salam zake Rais Malinzi amesema ushindi walioupata Twiga Stars katika mchezo huo wa awali, umetokana na maandalizi mazuri waliyoyapata chini ya kocha mkuu Rogasian Kaijage, benchi lake la ufundi na TFF.
Aidha Rais amewataka Twiga Stars kutobweteka kwa ushindi huo wa awali walioupata, bali wanapaswa kujiandaa vizuri zaidi kwa ajili ya mchezo wa marudiano ili waweze kupata ushindi na kuipeperusha vuzuri bendera ya Taifa ya Tanzania.
Mchezo wa marduiano unatarajiwa kufanyika kati ya April 10,11 na 12, 2015, huu jijini Dar es alaam na mshindi wa jumla atafuzu moja kwa moja kwenye fainali za Afrika kwa Soka la Wanawake (All Africa Games Women) zitakazofanyika Brazzavile Congo Septemba 3-18 mwaka huu.
Twiga Stars inatarajiwa kuwasili saa 7 kamili usiku (jumanne) jijini Dar es salaam kwa usafiri wa Shirika la Ndege la Ethiopia ikitokea nchini Zambia.
Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu , Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), watanzania wote wanawapa pongezi Twiga Stars kwa ushindi walioupata wa awali na kuwatakia maandalizi mema ya mchezo wa marudaiano.
Mabao ya Twiga Stars katika mchezo wa jana dhidi ya Zambia (The She-polopolo) yalifungwa na Asha Rashid (2), Shelder Boniface (1) na Sophia Mwasikili (1).
Share:

BAADA YA TIMU YA TANZANIA YA SOKA LA UFUKWENI KUTOLEWA NA MISRI INAREJEA LEO NYUMBANI


taifaaaaI
BEACH SOCCER YAREJEA LEO Wakati huo timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) inarejea leo mchana saa 8:45, kwa Shirika la Ndege la Ethiopia ikitokea nchini Misri ambapo jana ilipoteza mchezo wake wa marudiano kwa kufungwa 9-4 na wenyeji.
Rais Malinzi amesema timu ya Soka la Ufukweni haikupata matokeo mazuri katika mchezo wake kutokana na ugeni wa michuano hiyo, uzoefu ndio ulikuwa kikwazo kwa timu ya Tanzania, kwani ndio mara ya kwanza kushiriki michuano hiyo ikiwa ni miezi sita tangu kutambulishwa kwa mchezo huo nchini Tanzania.
Ili kuwa na timu bora ya Taifa na wachezaji wengi wa mchezo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limepanga kuutangaza na kuufundisha mpira wa ufukweni katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania, tofauti na sasa ambapo mchezo huo unachezwa Dar es salaam na Zanzibar.
Katika mchezo wa jana mabao ya Tanzania yalifungwa na Ally Rabbi (3) Kashiru Salum (1), Tanzania imetolewa kuwania kufuzu kwa fainali za Soka la Ufukweni barani Afrika na Misri kwa jumla ya mabao 15-6.
Misri imefanikiwa kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa Soka la Ufukweni Visiwa vya Shelisheli, zitakazofanyika mwezi April mwaka huu kwa mara ya saba mfululizo tangu kuanzishwa kwa mchezo huo mwaka 2006 nchini humo.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Share:

CHELSEA HAWAKAMATIKI YASHINDA KWA TABU 3-2 DHIDI YA HULL CITY ANGALIA TANO ZA JUU KWENYE MSIMAMO WA EPL

VINARA wa Ligi Kuu England Chelsea jana nusura wakose ushindi ugenini na Hull City baada ya kuongoza 2-0 na kuiruhusu Hull kusawazisha na Gemu kuwa 2-2 lakini Loic Remy alitoka Benchi na kuja kuwapa ushindi wa Bao 3-2.
Ushindi huu umeifanya Chelsea izidi kuongoza Ligi ikiwa Pointi 6 mbele ya Mabingwa Watetezi Man City lakini pia Chelsea wana Mechi 1 mkononi.
************,*********************
LIGI KUU ENGLAND
Msimamo-Timu za Juu
1. Chelsea Mechi 29 Pointi 67
2. Man City Mechi 30 Pointi 61
3. Arsenal Mechi 30 Pointi 60
4. Man United Mechi 30 Pointi 59
5. Liverpool Mechi 30 Pointi 59
************************************
Katika Mechi hiyo Bao za Chelsea zilifungwa na Eden Hazard Dakika ya 2 na DiegobCosta Dakika ya 9 huku Hull wakifunga Dakika za 26 na 28 kupitia Ahmed El Mohamady na Hernandez.
Bao la ushindi la Chelsea lilifungwa na Loic Remy alieingizwa kumbadili Diego Costa na kupachika Bao lake Dakika ya 77.
Kwenye Mechi nyingine ya Ligi Kuu England iliyochezwa  huko Loftus Road Everton iliichapa QPR Bao 2-1.
Bao za Everton zilufungwa Dakika za 18 na 77 na Seamus Coleman na Aaron Lennon likiwa Bao lake la kwanza kwa Everton tangu atue hapo kutoka Spurs.

Share:

EL CLASICO SUAREZ AISAIDIA BARCA KUIUA REAL MADRID JANA WAKISHINDA 2-1

BARCELONA wamepaa Pointi 4 mbele kileleni mwa La Liga baada ya ushindi wa 2-1 kwenye El Clasico dhidi ya Mahasimu wao wakubwa Real Madid kwenye Mechi iliyofanyika Nou Camp Jana Usiku.
Barca ndio waliotangulia kufunga katika Dakika ya 19 kwa Goli la Kichwa la Jeremy Mathieu alipounganisha Krosi ya Lionel Messi.
Real walisawazisha Dakika ya 31 baada ya Karim Benzema kumpa pasi ya kisigino Cristiano Ronaldo aliemchambua Kipa Bravo na kutikisa nyavu.
Hadi Mapumziko, Barca 1 Real 1.

Kipindi cha Pili Dakika ya 56, Dani Alves alipiga pasi ndefu na ya juu ya Mabeki wa Real, Pepe na Sergio Ramos, na kunaswa vyema na Luis Suarez aliemalizia vyema na kuipa Barca Bao la Pili na la ushindi.
Share:

Saturday, 21 March 2015

YANGA YAITANDIKA MGAMBO 2-0 HUKU NDANDA IKILAZIMISHWA SARE NYUMBANI NA JKT RUVU KESHO SIMBA NA AZAM WOTE DIMBANI

Yanga Leo wakiwa ugenini Uwanja wa mkwakwani Tanga  wameichapa Mgambo shooting magoli 2-0 na kuwaacha zaidi Mabingwa Watetezi Azam FC wakijiimarisha kileleni na kukamata hatamu ya Ligi Kuu Vodacom.
Bao za Yanga hii Leo zilifungwa na Simon Msuva dk 77 baada ya purukushani katika lango la Mgambo  na goli la pili ilikuwa  dk 83 Tambwe alipoifungia Yanga bonge la bao kwa kichwa baada ya krosi ya Msuva  
Hapa Mtwara katika uwanja wa  Nangwanda sijaona , wana wa kukaya NDANDA FC wametoa sare tasa yabila kufungana walipoikaribisha JKT RUVU kutoka mkoani pwani
Share:

LIGI KUU TANZANIA LEO NDANDA NA JKT RUVU HUKO TANGA FULL MVUA KOCHA WA YANGA AHOFIA KABLA YA KUWAVAA MGAMBO


Mvua inayoendelea kunyesha mjini Tanga inaonyesha kumpa hofu Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm.
Yanga inashuka dimbani leo kuwavaa Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Pluijm amesema anaingia hofu kabla ya kuivaa Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Mkwakwani leo kwa kuwa uwanja utakuwa kikwazo.

"Jana tulilazimika kusitisha mazoezi kutokana na mvua. Sasa leo imenyesha usiku wote na inaendelea. Kidogo inanitisha.

"Lakini sisi ni timu, tutalifanyia kazi suala hilo na kujua nini cha kufanya," alisema.

Jana, Yanga ilifanya mazoezi kwa dakika 40 kabla ya kusitisha kutokana na mvua kubwa kunyesha wakiwa mazoezi kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Share:

LA LIGA JUMAPILI HII NA EL CLASICO BIG MECHI BARCELONA VS REAL MADRID

Jumapil Vigogo wa Spain, Barcelona na Real Madrid, watavaana huko Nou Camp kwenye Mechi ya La Liga ambayo hubatizwa Jina la El Cladico na ambayo safari hii itakwenda mbali kutoa fununu ya Ubingwa na pia nania atazoa Pichichi.
Mechi hii inazikutanisha Barca wanaongoza La Liga wakiwa Pointi 1 mbele ya Real huku zote zimecheza Mechi 27 na kubakiza 11.
****************************
EL CLASICO- Uso kwa Uso:
-Barcelona ushindi 89
-Real Madrid ushindi 92
-Sare 48
*****************************
Katika Mechi yao ya kwanza Msimu huu, Real waliichapa Barca Bao 3-1 huko Santiago Bernabeu na tangu wakati huo hadi hivi karibuni walikuwa Vinara wa La Liga.
Lakini baada ya kukumbwa na Majeruhi na hasa kuumia kwa Beki Sergio Ramos na Viungo Luka Modric na James Rodriguez, Real wakaanza kupoteza mwelekeo na kushinda Mechi 3 tu kati ya 6.
Hapo ndipo Barca wakapata mwanya na kuitoa Real kileleni na wao sasa kuongoza Ligi wakiwa Pointi 1 Juu ya Real.
************************************
La Liga
Msimamo Timu za Juu
1. Barcelona Mechi 27 Pointi 65
2. Real Madrid Mechi 27 Pointi 64
3. Valencia Mechi 28 Pointi 60
5. Atletico Mechi 27 Pointi 55
************************************
Mbali ya sakata la mbio za Ubingwa kati ya Barca na Real pia zipo mbio za Pichichi, Tuzo ya Ufungaji Bora La Liga kati ya Mastaa wa Timu hizo, Lionel Messi wa Barca na Cristiano Ronaldo wa Real.
Hadi sasa Messi anaongoza akiwa na Bao 32 na Ronaldo ana Bao 30.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
BARCELONA (Mfumo 4-3-3):
-Bravo
-Alves, Pique, Mathieu, Alba
-Mascherano, Rakitic, Iniesta
-Messi, Suarez, Neymar
REAL MADRID (Mfumo 4-1-4-1):
-Casillas
-Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo
-Kroos
-Bale, Modric, Isco, Ronaldo
-Benzema

source; soka in tanzania
Share:

ANGALIA RATIBA YA MICHEZO YA UEFA DABI YA MADRID ATLETICO VS REAL MADRID

Droo ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI imefanyika Jana huko Nyon, Uswisi na Mabingwa Watetezi Real Madrid wamepambanishwa na Wapinzani wao wa Jadi Atletico Madrid ikiwa ni Marudiano ya Fainali ya Mwaka Jana ambayo Real walitwaa Ubingwa.
Kwenye Fainali hiyo Real walikuwa nyuma 1-0 hadi Dakika za Maheruhi na Sergio Ramos kuwasawazishia Real ambao walishinda 4-1 katika Dakika za Nyongeza na kutwaa Ubingwa.
Robo Fainali nyingine ni kati ya Paris Saint-Germain na Barcelona ambazo awali Msimu huu kwenye Mashindano haya zilikuwa Kundi moja na kila mmoja kushinda Mechi yake ya Nyumbani.
Pia Mwaka 2013 zilikutana kwenye Robo Fainali na Barca kusonga kwa ubora wa Magoli baada matokeo kuwa Jumla ya Mabao 3-3 kwa Mechi mbili.
DROO KAMILI:
**Mechi kuchezwa Aprili 14 na 15 na Marudiano ni Aprili 21 na 22
Paris Saint-Germain (FRA) v Barcelona (ESP)
Atletico Madrid (ESP) v Real Madrid (ESP)
Porto (POR) v Bayern Munich (GER)
Juventus (ITA) v Monaco (FRA)
Share:

KESHO JUMAPILI VITA KALI YA KUGOMBEA 4 BORA MANCHESTER UNITED VS LIVERPOOL

JUMAPILI Anfield utakuwapo mpambano mkali wa Mahasimu Liverpool na Manchester United ambao safari hii ukali wake umeongezwa zaidi na ile vita kali ya kugombea kufuzu 4 Bora ili Msimu ujao kucheza Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Timu zote zinatinga kwenye Mechi hii zikiwa kwenye fomu nzuri kwa Liverpool kushinda Mechi 5 mfululizo za Ligi Kuu England na Man United kushinda Mechi 3 mfululizo zilizopita.
Baada ya Liveroool kuchapwa 3-0 Uwanjani Old Trafford hapo Desemba 14 na Man United na kuachwa Nafasi ya 10 kwenye Ligi, Liverpool, chini ya Meneja Brendan Rodgers, hawajapoteza Mechi yeyote ya Ligi na sasa wapo Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Man United walio Nafasi ya 4.
************************************
USO KWA USO:
-Liverpool wameshinda Mechi 55
-Man United wameshinda Mechi 64
-Sare 44
************************************
Wakati Brendan Rodgers akipooza umuhimu wa Mechi hii ya Anfield na kudai bado zipo Mechi nyingi muhimu, Meneja wa Man United Louis van Gaal ametoa msisitizo kwa Wachezaji wake kudhibiti jazba hasa baada ya Timu yake kuathirika na Kadi Nyekundu dhidi ya Timu kubwa na hilo kumfanya awe Refa kwenye Mechi za Mazoezi ili kuwaonya Wachezaji wake.
Alipohojiwa kwa nini Kepteni wake Wayne Rooney huwa hafungi Anfield ambako mara ya mwisho kupiga Bao ni karibu Miaka 10 iliyopita, Van Gaal alisema ni kawaida kwa Mchezaji yeyote lakini anaamini hilo halitamwathiri Rooney kucheza vyema.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:l
LIVERPOOL (Mfumo 3-4-3):
-Mignollet
-Can, Skrtel, Sakho
-Allen, Gerard, Henderson, Moreno
-Sterling, Sturridge, Coutinho
 MAN UNITED (Mfumo 4-1-4-1):
-D Gea
-Valencia, Smalling, Jones, Blind
- Carrick
-Herrera, Fellaini, Mata, Young
- Rooney
REFA: Martin Atkinson
source:SOKA IN TANZANIA
Share:

Wednesday, 18 March 2015

ARSENAL WASHINDA 2-0 DHIDI YA MONACO LAKINI WATUPWA NJE ATLETICO NAO WASONGA MBELE WAKIITOA LEVERKUSEN KWA PENATI

Arsenal Jana Usiku iliichapa AS Monaco 2-0 kwao Stade Louis II Jijini Monaco ambako hawajafungwa tangu 2005 lakini wametupwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa Bao za Ugenini na hii ni mara ya 5 mfululizo kwa Arsenal kushindwa kutinga Robo Fainali.
Arsenal walifungwa kwao Emiratez Bao 3-1 na matokeo ya Jana kufanya Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili kuwa 3-3 na AS Monaco kutinga Robo Fainali kwa Ubora wa Bao za Ugenini.
Hii ni mara ya kwanza kwa AS Monaco kufika Robo Fainali tangu 2004.
Bao za Arsenal hiyo Jana zilifungwa na Olivier Giroid Dakika ya 36 na Aaron Ramsey, alietoka Benchi, na kufunga Dakika ya 79.
Katika Mechi nyingine iliyochezwa Jana huko Vicente Calderon Jijini Madrid, Wenyeji Atletico Madrid wametinga Robo Fainali kwa Mikwaju ya Penati 3-2 baada ya kufungana Mabao na Bayer Leverkusen 1-1 kwa Mechi mbili.
Leverkusen walishinda kwao Germany 1-0 na Jana Atletico kushinda 1-0 kwa Bao la Dakika ya 27 la Mario Suarez na kudumu hadi Dakika 90 kwisha na hivyo Mechi kwenda Dakika za Nyongeza 30 bila kubadilika.
Ndipo ikaja Mikwaju ya Penati 5 na Atletico kushinda Penati 3- 2 huku Antoine Griezman, Mario Suarez na Fernando Torres wakifunga na Raul na Koke wakikosa kwa upande wa Atletico wakati Leverkusen wafungaji ni Rolfes na Castro na Calhanoglu, Toprat na Stefan Kiesling wakikosa.
Atletico, ambao Msimu uliopita walifungwa Fainali ya Mashindano haya na Real Madrid, sasa wanaingia Droo ya kupanga Mechi za Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI itakayofanyika Ijumaa pamoja na A S Monaco, Real Madrid, FC Porto, Bayern Munich na Paris Saint-Germain.
Timu nyingine mbili za mwisho zitakazotinga Robo Fainali zitajulijana Leo baada ya Mechi kati ya Barcelona na Man City na ile kati ya Borussia Dortmund na Juventus.
Share:
Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates